ELIMU UJUZI BLOG NI BLOG YA JAMII AMBAYO NDANI YAKE KUNA ELIMU , UJUZI , UBUNIFU , MAFUNZO MBALIMBALI , UTAALAMU , STADI ZA MAISHA. AKIBA . UWEKEZAJI , UJASIRIAMALI , DINI , SAIKOLOJIA , TEOLOJIA , FALSAFA , NIDHAMU , ELIMU YA PESA , KUSOMA RIWAYA / HADITHI , USHAIRI , MICHEZO YA KUIGIZA . KARIBU UPATE MAARIFA UWEZE KUJIAJIRI NA KUFANIKIWA KATIKA MAISHA.
Monday, June 30, 2025
Saturday, June 28, 2025
Thursday, June 26, 2025
Saturday, June 7, 2025
Friday, June 6, 2025
Thursday, June 5, 2025
Tuesday, June 3, 2025
MAKALA : JENGA MIFEREJI MINGI YA PESA , UKIZIBA MMOJA MINGINE INATOA MAJI -----NA MWL. JAPHET MASATU ----CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Kakaa/Dadaa Yangu….
Hii ni siri lakini nitakudokezea…
Chanzo kimoja cha kipato ni kama mpenzi mwenye moods za ajabu.
Leo anakupenda.
Kesho anakusumbua.
Kesho kutwa anakudharau.
Na cha ajabu zaidi…
Wewe bado upo tu hapo, unamtegemea!
Sasa hebu jiulize:
Kama kazi yako itakoma leo, utaishije?
Kama biashara yako itakufa kesho, utaishije?
Kama mteja wako mkubwa atakata mawasiliano, utaanzia wapi?
Wewe ni kama mtu aliyepo kwenye ghorofa ya kumi,
na lifti imeshaanza kulegea…
Lakini bado unasema:
“Ah, bado ipo sawa tu.”
Tena ndo maana kila mwezi unatafuta chimbo la kukopa
Mwezi haujaisha, tayari unahangaika na maneno ya nitakulipa kesho.
Na unajua kabisa…
Ucheleweshaji wa kipato kimoja ni kama kufungiwa pumzi moja, hakuna backup.
Halafu kuna kauli za kuzima ndoto zako:
Ukianza biashara nyingine utachanganyikiwa…
Achana na mambo mengi… jipange na kimoja.
Kwanza vumilia hapo hapo hadi upate promotion.
Hahaaa!
Uvumilivu wa aina hiyo ni mzigo.
Na promotion ya kungojea miaka mitano ni matumaini hewa.
Leo vijana wenye akili timamu wana vyanzo vitatu hadi vitano.
Wanafanya kazi.
Wanauza online.
Wanafundisha watu.
Wanatoa huduma kwa bei nafuu.
Na wanaishi kama watu, sio mashine za kungojea mshahara.
Sasa sikiliza kaka, dada…
Unahitaji kujenga mifereji mingi ya pesa.
Ukiziba mmoja, mingine inatoa maji.
Ukikwama mahali, bado una uhakika wa kuishi bila stress.
Anza hivi:
Andika skills zako.
Tafuta hitaji kwenye jamii.
Tafuta njia rahisi ya kulifikia soko (mitandao ni msaada mkubwa).
Anza kutoa thamani.
Tumia muda wa jioni kujenga pesa ya kesho.
Ukiwa na simu yenye data, una bunduki mikononi.
Swali ni moja tu: Umeamua kuipigia kazi ama unaishikilia tu kama kijiti cha tambara?
Leo niko na jamaa mmoja, anaitwa Mushi.
Alikuwa mwalimu wa shule ya msingi.
Alikuwa anategemea mshahara mmoja kila mwezi shilingi laki nne tu.
Baada ya kukosa mshahara kwa miezi miwili, almost alipagawa.
Nikampatia kitabu hiki cha BIASHARA NDANI YA AJIRA,
Na nikamsaidia kujua namna ya kuandika ebooks kwa Kiswahili rahisi.
Leo hii:
Ana vitabu vinavyouzwa mtandaoni.
Ana group la Telegram linalotoa mafunzo ya malezi.
Anaanza kupata mialiko kufundisha mashuleni.
Anapata zaidi ya mshahara wake wa zamani na kwa uhuru.
Kila nikimcheki ananiambia:
Kipato kimoja ni kama kula chakula bila maji, kinakwama koo na kinahatarisha maisha!
Sasa ni zamu yako.
Acha kuwa mateka wa chanzo kimoja cha pesa.
Anza kuchimba visima vingine leo kabla jua halijazama.
Anza na ndoto zako.
Anza na muda wako mdogo.
Anza na simu yako.
Kama unataka kuungana na mushi kwenye safari ya kutengeneza vyanzo vingi vya kipato,
Usiogope kuanza vingi, ogopa kubaki na kimoja kinachokuteka.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
MWL. JAPHET MASATU , DAR ES SALAAM , TANZANIA --- EAST FRIKA -------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136