Showing posts with label MAKALA ZA MAISHA----NA MWL. JAPHET MASATU. Show all posts
Showing posts with label MAKALA ZA MAISHA----NA MWL. JAPHET MASATU. Show all posts

Tuesday, June 3, 2025

MAKALA : JENGA MIFEREJI MINGI YA PESA , UKIZIBA MMOJA MINGINE INATOA MAJI -----NA MWL. JAPHET MASATU ----CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

Kakaa/Dadaa Yangu….

‎Hii ni siri lakini nitakudokezea…

‎Chanzo kimoja cha kipato ni kama mpenzi mwenye moods za ajabu.
‎Leo anakupenda.
‎Kesho anakusumbua.
‎Kesho kutwa anakudharau.

‎Na cha ajabu zaidi…
‎Wewe bado upo tu hapo, unamtegemea!

‎Sasa hebu jiulize:
‎Kama kazi yako itakoma leo, utaishije?
‎Kama biashara yako itakufa kesho, utaishije?
‎Kama mteja wako mkubwa atakata mawasiliano, utaanzia wapi?


‎Wewe ni kama mtu aliyepo kwenye ghorofa ya kumi,
‎na lifti imeshaanza kulegea…
‎Lakini bado unasema:
‎“Ah, bado ipo sawa tu.”

‎Tena ndo maana kila mwezi unatafuta chimbo la kukopa
‎Mwezi haujaisha, tayari unahangaika na maneno ya nitakulipa kesho.
‎Na unajua kabisa…
‎Ucheleweshaji wa kipato kimoja ni kama kufungiwa pumzi moja, hakuna backup.

‎Halafu kuna kauli za kuzima ndoto zako:

Ukianza biashara nyingine utachanganyikiwa…
Achana na mambo mengi… jipange na kimoja.
Kwanza vumilia hapo hapo hadi upate promotion.

‎Hahaaa!
‎Uvumilivu wa aina hiyo ni mzigo.
‎Na promotion ya kungojea miaka mitano ni matumaini hewa.

‎Leo vijana wenye akili timamu wana vyanzo vitatu hadi vitano.
‎Wanafanya kazi.
‎Wanauza online.
‎Wanafundisha watu.
‎Wanatoa huduma kwa bei nafuu.

‎Na wanaishi kama watu, sio mashine za kungojea mshahara.

‎Sasa sikiliza kaka, dada…
‎Unahitaji kujenga mifereji mingi ya pesa.
‎Ukiziba mmoja, mingine inatoa maji.

‎Ukikwama mahali, bado una uhakika wa kuishi bila stress.

‎Anza hivi:
📍 Andika skills zako.
📍 Tafuta hitaji kwenye jamii.
📍 Tafuta njia rahisi ya kulifikia soko (mitandao ni msaada mkubwa).
📍 Anza kutoa thamani.
📍 Tumia muda wa jioni kujenga pesa ya kesho.

‎Ukiwa na simu yenye data, una bunduki mikononi.
‎Swali ni moja tu: Umeamua kuipigia kazi ama unaishikilia tu kama kijiti cha tambara?

‎Leo niko na jamaa mmoja, anaitwa Mushi.
‎Alikuwa mwalimu wa shule ya msingi.
‎Alikuwa anategemea mshahara mmoja kila mwezi shilingi laki nne tu.

‎Baada ya kukosa mshahara kwa miezi miwili, almost alipagawa.
‎Nikampatia kitabu hiki cha BIASHARA NDANI YA AJIRA,

‎Na nikamsaidia kujua namna ya kuandika ebooks kwa Kiswahili rahisi.
‎Leo hii:
📚 Ana vitabu vinavyouzwa mtandaoni.
👨‍🏫 Ana group la Telegram linalotoa mafunzo ya malezi.
🎤 Anaanza kupata mialiko kufundisha mashuleni.
💸 Anapata zaidi ya mshahara wake wa zamani na kwa uhuru.

‎Kila nikimcheki ananiambia:
Kipato kimoja ni kama kula chakula bila maji, kinakwama koo na kinahatarisha maisha!

‎Sasa ni zamu yako.
‎Acha kuwa mateka wa chanzo kimoja cha pesa.
‎Anza kuchimba visima vingine leo kabla jua halijazama.

‎Anza na ndoto zako.
‎Anza na muda wako mdogo.
‎Anza na simu yako.

‎Kama unataka kuungana na mushi kwenye safari ya kutengeneza vyanzo vingi vya kipato,



‎Usiogope kuanza vingi, ogopa kubaki na kimoja kinachokuteka.

‎Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

MWL.  JAPHET    MASATU , DAR  ES  SALAAM , TANZANIA ---  EAST    FRIKA -------CALL  /  SMS   /  WHATSAPP  +  255  716 924 136 


Friday, May 2, 2025

JE , MSHAHARA WAKO WA KILA MWEZI WA KUTOSHA ???? UTAISHI UKIFUKUZA MAISHA MPAKA UNAZEEKA ------ ????

 Mpendwa Rafiki,

‎Unajua nini kinauma kuliko mshahara mdogo?

‎Ni kuwa na mshahara lakini bado unaishi kama huna kazi.

‎Kila mwezi hela zinaingia… lakini hazikai.

‎Kila siku unasema, Mwaka huu lazima nibadili maisha… lakini bado umerudi palepale.

‎Unajituma kazini, unachoka, lakini mafanikio yako bado yako pending!

‎Halafu cha ajabu… watu walioanzisha biashara wakiwa bado kwenye ajira, leo hii wameanza kuamua hata siku ya ku-resign.

‎Wewe bado unaota tu, “siku moja…”
‎Siku moja haiji bila hatua, bro!

‎Ngoja nikuambie ukweli mchungu lakini wa maana…

‎Kama hujui kudili na pesa zako, hujui kupangilia muda wako vizuri, hujui kujiwekea direction ya mafanikio hata upewe mshahara mara mbili, bado utalia.

‎Utaishi ukifukuza maisha mpaka unazeeka.

ENDELEA   KUJIFUNZA    MENGI    NDANI YA    HII    BLOG  INAYOITWA     ELIMU    UJUZI  TANZANIA  BLOG  

INAYOENDESHWA    NA   MWL  .  JAPHET   MASATU--  

WA   DAR  ES   SALAAM  ,   TANZANIA ,   AFRIKA    YA  MSHARIKI  TUWASILIANE   KWA  CALL   /   SMS   /  WHATSAPP   +  255  716  924 136

WHATSAPP NUMBER