Monday, May 12, 2025

MAKALA : UTULIVU , AMANI , FURAHA , UPENDO HAVIUZWI DUKANI VIPO NDANI YAKO , VIFUKUE UFURAHIE MAISHA---KUWA NA TAHAJUDI ( MEDITATION ) KILA SIKU KWA DAKIKA 5 .10 . 15 INATOSHA-------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

 Kakaa/Dadaa…

‎Hivi unajua ni kwa nini kila siku unaamka umechoka hata kama ulilala masaa 8?

‎Kuna kitu kimoja tu kinakusumbua… akili yako haipumui.

‎Una mawazo mengi.

‎Stress.
‎Presha.

‎Mengine hata hujui yanatoka wapi.
‎Lakini yanakutesa.

‎Unasema huna muda.
‎Unasema maisha ni magumu.
‎Unasema nitapumzika nikiwa kaburini.

‎Lakini ukweli ni huu:
‎Ukikosa utulivu ndani yako…
‎Hakuna utakachofanikisha nje yako.

‎Sasa Tuseme Ukweli Wote….

‎Unajitesa Mwenyewe.

‎Umezoea kukimbizana na kila kitu.

‎Simu haikai mbali.

‎TV haizimwi.

‎Instagram haifungwi.

‎Magroup ya WhatsApp hayanyamazi.

‎Hali hii inakuua polepole.

‎Inakuondolea amani.

‎Inakurudisha nyuma.

‎Na mbaya zaidi…

‎Unadhani hiyo ndiyo kawaida ya maisha.

‎Achana Na Uongo Wa DUNIA.

‎Watu wengi hawajui siri hii…

‎Kuna njia moja rahisi sana ya kupata amani ya ndani.

‎Ya kutuliza kichwa.

‎Ya kujisikia safi hata ukiwa huna kitu.

‎Inaitwa tahajudi (meditation).

‎Dakika 10 tu kwa siku zinaweza kubadilisha kila kitu.

‎Watu wanasema…
‎“Ah hiyo ni ya Waasia.”
‎“Ni mambo ya yoga.”
‎“Ni mapepo.”

‎Lakini siyo kweli.

‎Tahajudi ni tiba ya kiroho, kiafya, na kisaikolojia.

‎Ni nafasi ya kuongea na nafsi yako.
‎Kusafisha akili yako.

‎Kusikiliza kilicho ndani yako..

‎Jifunze Kitu Hapa….

‎Meditation haichukui muda.
‎Haitaki pesa.

‎Haibagui dini wala elimu.

‎Unakaa tu kimya. Unavuta pumzi. Unawaza kwa utulivu.

‎Dakika 5. 10. 15.
‎Inatosha.

‎Kila siku.
‎Polepole, unajiona mtu tofauti.
‎Unaanza kuelewa maisha.
‎Unaanza kuishi kwa amani.

‎Ndiyo dawa ya wasiwasi.
‎Ndiyo suluhisho la stress.
‎Ndiyo siri ya watu wenye mafanikio makubwa.

‎Mimi Niliwahi KUPOROMOKA KISAIKOLOJIA.

‎Na nitakuambia ukweli huu…

‎Miaka michache iliyopita, maisha yalinigonga mkwara.

‎Nilikuwa nimechanganyikiwa.

‎Mara deni, mara pressure, mara msongo, mara mahusiano hayajakaa vizuri.

‎Siku moja nikakaa chini. Nikasema, Acha nijaribu hii tahajudi.

‎Nilikaa kimya. Nikavuta pumzi.
‎Nilianza polepole.

‎Siku ya kwanza… hakuna nilichosikia.
‎Siku ya pili… niliboreka.
‎Siku ya tatu… nililia.
‎Siku ya saba… nilitulia.

‎Na tangu siku hiyo…
‎Maisha yamebadilika.
‎Sina presha ya maisha.

‎Nimejifunza kujisikiliza.
‎Nimejifunza kuwa mtulivu hata dunia ikiwa inateketea.

‎Na leo, najisikia kuwa hai kwa mara ya kwanza.

‎Mwisho Wa SIKU…

‎Usubiri msiba ndipo uanze kujitafuta.
‎Usingojee maisha yakuchoshe kabisa ndio uanze kutafuta utulivu.

‎Anza leo.

‎Kaa chini.
‎Fumba macho.
‎Vuta pumzi.
‎Futa mawazo.
‎Sikiliza moyo wako.

‎Hapo ndipo utagundua kuwa utulivu hauuziwi upo ndani yako.

No comments:

Post a Comment

WHATSAPP NUMBER